IMANI NA MAOMBI
UHUSIANAO WA IMANI NA MAOMBI.
UTANGULIZI:
IMANI NINI? Imeandikwa
WAEBRANIA 11:1 "Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo ni bana ya mambo yasiyoonekana."
Yesu ndiye mwanzo wa imani imeandikwa LUKA 17:5 "Mitume wakamwambia Bwana tuongezee imani." WARUMI 10:17 yasema "Basi imani chanzo chake ni kusikia na kusikia huja kwa neno la kristo."
Imani ya haki ni kuamini yote ambayo Yesu ametutendea. imeandikwa WARUMI 5:1 "Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na imani kwa Mungu kwa njia ya Bwana wetu Yesu kristo."
Imani ni kuwa na imani kwa Mungu katika mambo yote. imeandikwa WAEBRANIA 10:38 "Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani naye akisita-sita Roho yangu haina furaha naye."
Imani dhaifu yaweza kuwa yenye nguvu Mungu akimsaidia imeandikwa MARKO 9:24 "Mara babaye yule kijana akapaza sauti akasema Naamini nisaidie kutokuamini kwangu."
Mwombaji yeyeote ili awe na nidhamu katika Maombi ni lazima atambue uhusiona wa Maombi na imani.
LUKA 18:1,8
Katika mistari hii ukitazama katika mstari wa nane kuna maana ya kipekee ambayo inaonesha kuwa IMANI ni mkono wa kupokelea kile unacho kiomba kwa Mungu.
Yesu ana sema na sisi kuwa yatupasa kuwa waombaji wenye bidii na bila kuwa na kikomo na kutokukuta tamaa
LUKA 18:2-6,mwanamke mjane hakukata tamaa katika kutafuta haki yake na ndio maana alienda kila mara kufuatilia haki yake hadi akapokea.
Kukata tamaa ni kupoteza mkono wa kupokea kile unachoomba. Hivyo ni muhimu kutambua kuwa ile imani uliokuwa nayo wakati unaomba haitakiwi kupotea mpaka upokee.
MATHAYO 17:20-21
Katika mistari tunajifunza kuwa imani yaweza kuongezeka kwa kuomba, hivyo Maombi yanaongeza kiwango cha imani.
Kuwa mtu wa imani au mwombaji mwenye tabia ya imani ni muhimu sana, maana imani inawezesha kupokea yale unayoomba kwa Mungu
Biblia inaseam kuwa “kwa kadri ya imani yenu mpate” MATHAYO 9:27-31
KADRI inamaanisha kiwango au kipimo; kwa hiyo unapata utakacho kwa kiwango cha imani ulio nayo.
MATHAYO 15:22-28, MATHAYO 8:10
Katika maisha Maombi kama majawabu ya Maombi unayoyapata hayakuridhishi jambo la kwanza chunguza kiwango cha imani yako kikoje, hivyo fanya juhudi na kujibidisha sana katika kulisoma Neno la Mungu na kulifanyia kazi, pia kuwa na bidii katika Maombi na tena ongeza na Maombi ya kufunga, ili ufikie kiwango cha kuona mambo makubwa yakitendeka.
MARKO 11:23-24….yoyote tuombayo ,na kuwa na imani tutayapokea.
Imani si kitu cha wakati Fulani , imani ni sasa yaani inatupasa kuamini sasa sio baadaye. Ukiomba unapokea kwa imani .
Kunatofauti ya tumaini na imani;
Tumaini ni tarajio la jambo Fulani(hope is expectation of something)
1KORINTHO 13:13
Mstari huu unaonyesha jinsi imani inavyotofautiana na tumaini na ni vigumu kuweka imani mahali pa tumaini, unaposema nitapokea moja kwa moja hilo ni tumaini ulilo nalo na sio imani.
Maombi ya imani yanahitaji pale unapo maliza kuomba moja kwa moja uamini kuwa umepokea na sio utapokea.
Ukiwa kama mtu wa Maombi ni lazima uweke imani yako kwa Yesu Kristo na sio kwa mazingira yanayokuzunguka.
2KORINTHO 5:7 ….maana twaenenda kwa imani si kwa kuona, macho yanasaidia kuona yanayo onekana bali imani inakusaidia kuona yale yasiyoonekana 2KOR 4:18
Kama mwombaji ni muhimu kutambua kuwa vile vinavyoonekana vimetokana na vile visivyoonekana kwa macho ya nyama, na ndio maana unapomwomba Mungu hutarajii akujibu kwa njia moja kwa sababu yeye hutumia njia mbalimbali kuleta majibu ya Maombi yako.
Kwa mfano katika anga la mahali ulipo kuna vyombo vya habari vya aina tofauti tofauti kama vile BBC,TBC,ITV,RADIO MBALIMBALI N.K..Lakini hazionekani kwa macho ya kawaida mpaka uwe na chombo chenye uwezo wa kunasa hayo mawimbi ndipo uweze kuona au kusikia,
Na ndivyo ilivyo katika ulimwengu wa Roho kuna majibu ya kila ombi ambalo unaliomba kwa Bwana ingawa halionekani, lakini ukiwa na Imani unapokea kile ambacho umekuwa ukiomba. Ili kuwa na msingi mzuri wa Maombi yenye majibu ni lazima Maombi yaanzie kwenye neno la mungu maana neno ndilo msingi wa imani, na kile ambacho Mungu amesema lazima atakitimiza. Maombi ya imani yatakufanya kupokea chochote kile ambacho unakihitaji kutoka kwa Mungu, ikiwa tu kimejengwa katika msingi wa Neno la Mungu ambalo ndilo mapenzi yake.
IMANI NI MKONO WA KUPOKELEA MAJIBU TOKA KWA MUNGU.
Maoni
Chapisha Maoni